Tuesday, November 13, 2012

Fahamu Footprint Digital......

Footprint( Nyayo) kila mmoja wetu akitembea anaacha alama ardhini au sakafuni lakini......
Footprint digital ni rekodi ya mambo yote umefanya kwenye mtandao. Hii ni pamoja na kila kitu una Googled na YouTubed, maoni yote uliyoyaandika na webpages (Tovuti) zote ulizowahi kutazama. Ni muhimu kuwa makini kwenye mtandao, kwa sababu unaweza kuwa spotted (gundulika) kwa kufanya mambo yasiyofaa.

Muda gani data hizi  huhifadhiwa? 

Milele! Hivyo kuwa makini. Hata kama waweza futa historia yako katika Browser mfano (Opera, Mozilla,internet Explorer,safari n.k) bado inaweza kutazamwa.

Kwa nini unahitaji kuwa makini wakati wa kuandika kwenye mtandao?
unachokiandika leo kinaweza kukugharimu siku zijazo kama kitakuwa si kizuri. siku hizi wamiliki wengi wa makapuni au waajiri wamekuwa wakiangalia rekodi ya watu wanaotaka kuwaajiri kupitia mitandao ya kijamii. mf Facebook.

kuthibitisha hili Jaribu kugooggle Jina lako huone nini kina tokea
 

Unatumia muda mwingi kwenye mtandao, Nani ana kuangalia?
Wamiliki wa tovuti wanaweza kupata habari zako. Pia mtu yeyote anaye tumia kompyuta yako au kifaa anaweza kuona historia.

 

Ni taarifa gani huhifadhiwa juu ya kila mmoja wetu mtandaoni?
taarifa zote za kila tovuti unayotembelea, (comment)maoni unayotoa, (Poll) kiwango, au barua pepe huhifadhiwa.

0 comments:

Post a Comment