Friday, November 2, 2012

HATUA ZA KUFANYA HARAKA PINDI UNAPO MWAGA KIMIMINIKA KATIKA KOMPYUTA YAKO



Mara ngapi Umewahi mwaga kinywaji/kimiminika katika  computer yako..? 

kama tayari na kitu pekee kuharibika ilikuwa ni keyboard  jihesabu mwenye bahati. Mara nyingi baadhi ya watumiaji wa kompyuta wamekuwa  na tabia ya kuweka au kunywa vimiminika (vinywaji) mfano. Kahawa,chai,Soda,maji, bia,juisi katika meza  wanazotumia kompyuta zao.

Kwa bahati mbaya vimiminika na umeme havipatani. Suluhisho.  Epuka kunywa au kuweka vimiminika  karibu na kompyuta yako.



Fanya yafuatayo kama ukimwaga kiminika katika kompyuta yako. Zima haraka kisha Tenganisha kompyuta na umeme. kwa kuchomoa nyaya katika soketi za umeme. Kama ni desktop kompyuta fungua na utenganishe power supply na motherboard. Kama kuna majimaji. Pangusa/ futa kwa kitambaa kikavu au kama kitu ulichomwaga kina natanata unaweza tumia kitambaa kibichi kusiaidia kuondoa mabaki na kisha tumia kikavu. 

Ukimaliza weka sehemu yenye hewa kwa muda wa siku 2 maka 3 ili kuruhusu unyevunyevu kutoka, hakikisha mpaka imekauka vizuri ndio unaweza kuwasha tena kompyuta yako.
Kama ni Laptop. Zima haraka kisha toa betrii na uiache wakati unasubiri kupeleka kwa fundi.





0 comments:

Post a Comment